BAADA ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Simba,
aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya City, Kibu Denis sasa ameanza na programu
maalum ya mazoezi ya Gym kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea msimu ujao wa
2021/22.
Inaelezwa kuwa tayari Kibu amekamilisha kila kitu na Simba kwa
ajili ya kuwatumikia msimu ujao, na sasa anasubiri kutambulishwa rasmi kwa
Wanasimba ili aanze kukitumikia kikosi hicho.
Kibu amesajiliwa Simba kama pendekezo la kocha mkuu wa klabu
hiyo, Didier Gomes ambapo anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya
timu hiyo, ambayo inatajwa iko kwenye mpango wa kuachana na straika mmoja.
Akiwa na Mbeya City Kibu msimu uliopita Kibu alifanikiwa
kuonyesha uwezo mzuri kiasi cha kuhusika kwenye zaidi ya mabao manne, na kupata
nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichocheza dhidi ya Malawi.
Kuhusu usajili wake Kibu amesema: "Nipo Dar es
Salaam kwa ajili ya kukamilisha usajili wangu kwenye klabu moja kubwa,
tuendelee kusubiri kila kitu kitawekwa wazi hivi karibuni.”







0 COMMENTS:
Post a Comment