August 18, 2021


 BALAMA Mapinduzi, kiungo mshambuliaji wa Yanga tayari ameshaanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiweka sawa na msimu ujao wa 2021/22.

Nyota huyo ambaye anakumbukwa na mshikaji wake Aishi Manula kwa kumtungua bao la nje ya 18 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Januari 4,2020 alikuwa nje kwa muda akitibu majeraha ya funda la mguu.

Kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ulikuwa ni wa kukata na shoka kwa kuwa Simba ilikuwa inapewa nafasi ya kushinda baada ya kufunga mabao mawili ya kuongoza yaliyofungwa na Meddie Kagere kwa penalti pamoja na Deo Kanda. 

Aliumia kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC.


Kutokana na tatizo hilo alikuwa nje kwa msimu mzima wa 2020/21 akitibu majeraha yake na aliweza kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.

Taarifa kutoka nchini Morocco zimeeleza kuwa nyota huyo ameanza mazoezi ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Yanga imeweka kambi kwa muda nchini Morocco na inatarajiwa kurejea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya Mwananchi Day inayotarajiwa kufanyika Agosti 29. Uwanja wa Mkapa.


2 COMMENTS:

  1. Ilianza Simba Day na baadae ikafata Mwananchi Day, safi kabisa

    ReplyDelete
  2. Yaa hata yanga ikaanza badae simba ikaundwa kutoka kwa yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic