UONGOZI wa Kagera Sugar umeweka wazi kuwa mabosi wa Simba walionyesha dharau kubwa kwenye usajili ya mchezaji wao Yusuph Mhilu ambaye amesaini dili la miaka mitatu ndani ya Simba.
Ofisa Habari wa Kagera Sugar, Hamis Manzanzala amesema kuwa mabosi hao wameonyesha darau tatu ikiwa ile dharau ya kwanza wamefanya mazungumzo na mchezaji bila idhini yao, pili wamemsainisha mchezaji mkataba bila idhini yao,tatu wamemtangaza Yusufu Mhilu bila idhini yetu huku ni kutudharau.
“Mhilu alikuwa anamkataba na sisi wa mwaka mmoja kubaki na katika mkataba wake kulikuwa na kipengele cha kusajili na kumtumia mdogo wake Dickson Mhilu kitu ambacho tulikifanya, Simba hawawezi kumtumia Mhilu mpaka sisi tuamue.
“Wao wameshamsainisha Mhilu sasa wanakujaje kutaka kufanya mazungumzo, tumeingia gharama kubwa kumtengeneza Yusuph Mhilu gharama yake ni kubwa.”
Chanzo:RFA
Duuh,mbona sa hii nayo shidaaa???
ReplyDeleteKwani TFF walishatoa orodha ya mwisho ya wachezaji waliosajiliwa na timu za ligi kuu 21/22? Vipi kama Simba watalikata Jina la Yusufu Mhilu katika orodha yao ya mwisho itakayokwenda TFF? Kwa sababu usajili wa ndani bado unaendelea. Kagera kama wameingia tamaa ya kutaka kupata pesa nyingi wanatakiwa kuwa na adabu katika madai yao la sivyo wanaweza kukosa yote. Kwa sababu Kama simba wataachana na Muhilu, Kagera wasitarajie kuwa na mhilu atakaekuwa na Mapenzi na timu yao.
DeleteHujitambui eti hata sheria za usajili huzijui. Pole yako
DeleteYan we mavi ya mwisho kwel yan ile kumtangaza mtu akiwa na mkataba wa timu nyngne hyo n jinai haf we unasema et watakosa vyote duu watu inaonekana hamjui mpira unaazia wap na kuishia wap
DeleteCAS tarehe 24 washuke tu daraja wamezoea tabia mbovu
ReplyDeleteHashuki mtu daraja weye
DeleteSemwni gharama yake ni ipi mpewe, msiogope
ReplyDeleteWastabu wana msemo wa "kun faya khun" yaan "ukitenda utatendwa"!
ReplyDeleteSimba walimfukuza Hassan Kessy kwamba aliwafungisha; wakawa hawamtumii. Alipojiunga na Yanga na kusafiri na Timu kwenda Uturuki, Simba walikuja juu wakidai Hassan Kessy ni mchezaji wao na bado alikuwa na miezi 6 kwenye mkataba. Sekeseke lake lilikuwa zito kiasi, Yanga wakapigwa faini na Kessy akafungiwa! Imenikumbusha muziki wa Dar Jazz "Yamewakuta wenzetu", sasa mtendwa katenda yeye!!
Nasubiri kuuona ujasiri na ukakamavu wa TFF hii mpya kama kweli kumbukumbu wanazo
Yataisha hakuna shaka
ReplyDeleteKhasani kesy laana ya simba mpaka leo yupo yupo tu.
ReplyDeleteKwani Simba ndio watoa riziki? Hata Simba ikimuacha Mhilu tayari kikanuni imekiuka kumsainisha na kumtambulisha mchezaji mwenye contract na timu nyingine. Wacha mnyoke walaghai wakubwa nyie
ReplyDeleteMikia bado wanaendesha mambo yao kienyeji sana. Tutaona kama ushifta wa kupindisha mambo wa fff utaendaje
ReplyDeleteSimba 1 Morrison Rabat 1
ReplyDeleteMikia fc hahaha hiyo ndo NEXT level!
ReplyDeleteSimba. 2.Rabat. 2
ReplyDeleteKwann ufanye usajili wa kuibiana wachezaji? Hawa viongozi wa Simba wana matatizo gan? Next level gan ya upuuzi wa miaka ya 70?
ReplyDeleteMuungwana hawafanyi mambo bila utaratibu, pia TFF wasiwaonee haya hii sasa imekua too much
SASA KAMA MCHEZAJI HATAKI KUCHEZA KAGERA SUGAR? UTAMLAZIMISHA. MHILU AMESHAFUNGUA SHAURI LA KUVUNJIWA MKATABA KWANINI WAO WANG'ANINIE? MHILU HAWEZI KURUDI KAGERA KAMWE.
ReplyDeleteYataisha nothing will go wrong
ReplyDeleteVipi wakimalizana Simba na Kagera Sugar, kuna kosa Simba ataadhibiwa na TFF?
ReplyDelete