AKIWA na umri wa miaka 26 ameweza kunyanyua makwapa mara nne akiwa na timu tofauti baada ya kushinda mataji makubwa na kumfanya awe na furaha kwa wakati huo.
Ni Kepa Arrizabalaga ambaye aliletwa duniani Oktoba 3,1994 ni raia wa Hispania ambapo anacheza timu ya taifa ya Hispania kwa nafasi ya mlinda mlango.
Rekodi zinaonyesha kuwa taji lake la kwanza alitwaa mwaka 2013 nchini Hispania na ilikuwa ni lile la European U 19. 2018/19 alinyanyua makwapa kwa kutwaa taji la Europa League.
Msimu wa 2020/21 akiwa ni mali ya Chelsea alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa chini ya Kocha Mkuu, Thomas Tuchel na alikuwa shujaa katika fainali ya UEFA Super Cup baada ya kuokoa penalti mbele ya Villarreal na Chelsea ilishinda kwa penalti 6-5.
Akiwa na timu yake ya taifa ya Hispania aliweza kushiriki Kombe la Dunia 2018 mara moja. Mkataba wake unameguka Juni 30,2025 ndani ya Chelsea ambapo alijiunga na timu hiyo Agosti 8,2018.
0 COMMENTS:
Post a Comment