August 10, 2021

 


KIUNGO Jimmy Ukonde ambaye alikuwa kwenye majaribio ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa anaamini kwamba atacheza ndani ya timu hiyo msimu ujao kikosi cha kwanza.

Nyota huyo alikuwa chini ya Kocha Mkuu, Razack Siwa ambaye alipewa jukumu la kusimamia timu hiyo kwenye mashindano ya Kombe la Kagame alicheza mechi tatu na kuonyesha makeke licha ya timu hiyo kutolewa katika hatua ya makundi.

Ukonde alisema kuwa timu ambazo walikutana nazo zilitumia makosa yao kupata ushindi jambo ambalo limewafanya waondelewe mapema jambo ambalo hawakupanga.

“Imani yangu ni kuona kwamba msimu ujao nitakuwa ndani ya Yanga. Nitacheza kwa sababu ninaweza na kila kitu kinawezekana.

“Hatukupanga kutoka mapema lakini timu ambazo tulikutana nazo pia zilikuwa zinahitaji matokeo jambo ambalo limefanya tuondolewe kwenye mashindano.

2 COMMENTS:

  1. Wa kawaida sana wewe jamaa

    ReplyDelete
  2. Kocha wetu ni mzuri sana na anajua nani anatakiwa kucheza sehemu gani na hutoa nafasi kwa kipa mchezaji anaweza kutufaa sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic