August 6, 2021


 NIMEKUJA kufanya kazi.” ndilo neno pekee ambalo amelisema mshambuliaji mpya wa Klabu ya Yanga, Heritier Makambo tena kwa msisitizo mkubwa baada ya kusaini mkataba na kutambulishwa kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo.

 

Makambo amerejea katika kikosi cha Yanga baada ya kufikia makubaliano ya kuachana na Klabu ya Horoya ya Guinea, aliyojiunga nayo mwaka 2019 kufuatia changamoto za uhusiano wake na kocha wa timu hiyo.

 

Nyota huyo inaelezwa kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia Yanga.Akiwa na Yanga msimu wa mwaka 2018/19 Makambo aliifungia klabu hiyo mabao 17, na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye chati ya wafungaji bora kinara akiwa, Meddie Kagere wa Simba aliyetupia mabao 23 kisha Salim Aiyee ambaye ni mzawa alikuwa nafasi ya pili kwenye chati ya ufungaji.

 

Alipoombwa kuzungumza chochote baada ya utambulisho huo, Makambo hakutaka kuwa na maneno mengi ambapo alisema kwa kifupi: “Siwezi kuzungumza kitu kwa sasa zaidi ya kuwaahidi Wanayanga kuwa nimekuja kufanya kazi, na kuisaidia Yanga kushinda makombe," .

 

Makambo aliyatamka maneno hayo mbele ya Injinia Hersi ambaye pia alizidi kumsisitiza kuhusiana na umuhimu wa kuwarejeshea Wanayanga furaha.

 

Naye Kaimu Katibu mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa alizungumza mambo mbalimbali kuhusu usajili unavyokwenda klabuni hapo.

 

“Bado hatujamaliza usajili, tutaendelea kushusha majembe mapya kutoka nje ya nchi lakini pia, nyota mbalimbali wazawa katika malengo ya kuhakikisha tunakuwa na kikosi bora zaidi na imara kwa msimu ujao.

 

"Wapo wachezaji tunaohusishwa nao lakini nisingependa kuzungumza hayo kwa sasa, tutawaweka wazi pale kila kitu kitakapokuwa tayari.


Kwetu malengo makubwa ya kufanya usajili huu ni kuhakikisha tunarejesha furaha ya mashabiki wa Yanga, kwa kushinda makombe katika michuano ambayo tutashiriki mwakani.

 

"Kila mnachokiona katika usajili huu ni mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi, tunataka mpaka atakaporudi akute ripoti aliyoiacha imekamilika, lakini pia tumekuwa tukimuhabarisha katika kila hatua ambayo tumefikia.”

6 COMMENTS:

  1. Hata Sarpong na Fiston walikuwa na maneno maneno kama hayo ya kwenye kanga, kushinda mitandaoni kuposti posti picha na vijimisemo kibao, Fiston anashinda saluni kubadili rangi za nywele badala ya kufanya mazoezi kazi yake ilikuwa ni kuweka blitch nywele kama mrembo fulani, huku Sarpong ni kupiga picha za location mbali mbali kama muuza sura kwenye majarida ya urembo na fashion, uwanjani ni kujiangusha angusha kutupa tupa mikono na kushangilia magoli yaliyo fungwa na mabeki bila hata aibu, maneno meeeeeeengi vitendo hamna. Makambo wewe ni GARASA punguza maneno tulia ujifunze kwa vitendo kazi wafanyayo kina Kagere, Mugalu , Bocco nk hawa jamaa sio watu wa mdomo mdomo ni watu wa vitendo tu. Sijawahi msikia Prince Dube wa Azam akiongea ongea hovyo ila Sarpong na Fiston utadhani wanashinda Studio.

    ReplyDelete
  2. Ulitaka wakuambieje ili wewe ufurahi?

    ReplyDelete
  3. Makambo hana jipya misimu yote akikaa2 bench

    ReplyDelete
  4. Kwani Makambo kaongea ovyo? Au unateseka na ujio wake?

    ReplyDelete
  5. Makambo aalikuwa kama alivokuwa Mkude na Ajib

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic