August 3, 2021

 NTOTA Peter Banda amesema kuwa kwa sasa yupo Msumbiji na awali ilipaswa aje na timu ya Big Bullets Bongo ila mambo yalikwenda tofauti.


Big Bullets ambayo ni timu yake ipo Tanzania ikishiriki mashindano ya Kagame na Agosti Mosi iligawana pointi mojamoja na Yanga baada ya kupata sare ya kufungana bao 1-1.


Habari zinaeleza kuwa Simba wapo kwenye hesabu za kuinasa saini yake huku Yanga nao wakitajwa kuingilia kati dili hilo.


Jana alikuwa anapewa nafasi ya kutambulishwa ndani ya Simba ila mambo yalikwenda tofauti na hakuweza kutambulishwa.


 Kwa sasa inaelezwa kuwa alipelekwa Kigamboni kumalizana na mabosi wa Yanga ambao waliamua kuwazunguka watani zao Simba ambao walikuwa wanapewa nafasi ya kumpa dili nyota huyo.


Banda mwenyewe amesema kuwa yupo Malawi ila aliweka wazi kuwa alikuwa anawasiliana na viongozi wa Simba ambao walikuwa wanahitaji kumpa ofa mshambuliaji.

Kuhusu usajili wa Yanga, Ofisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli alisema kuwa wanakwenda kimyakimya na wachezaji watakaokamilisha madili watatambulishwa.

4 COMMENTS:

  1. FAKE NEWS NI NYINGI KWASASA SIO BANDA WALA AUCHO ALIYESAJILIWA YANGA HUU NI WAKATI WA “KUWARUSHA ROHO “ MASHABIKI

    ReplyDelete
  2. Hatupendi upuuzi.uzinguaji mwingine haufai kabisa hbr za kutunga hizi ni ugoro mtupu

    ReplyDelete
  3. WATU WANAHANGAIKA KUPATA HELA, WANAJIWEKEA BUNDLE HALAFU MNALETA HABARI ZISIZO NA UHAKIKA, INAUMIZA SANA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic