NYOTA wa timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 23, leo Agosti 2 ni kumbukizi yake ya kuletwa duniani.
Kiungo huyo ambaye ni hazina ya taifa la Tanzania alikuwa miongoni mwa kikosi cha U 23 kilichorejea na taji la Cecafa Challenge 2021.
Tanzania ilishinda mbele ya Burundi katika mchezo wa fainali uliochezwa nchini Ethiopia.
Chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen, vijana wa U 23 waliweza kutwaa taji hilo ikiwa ni furaha kwa wachezaji na taifa la Tanzania kiujumla.
Kila la kheri mpambanaji wa Tanzania, maisha mema. Mungu azidi kukulinda.
0 COMMENTS:
Post a Comment