August 5, 2021


 NI mfungaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ametupia mabao 16 na pasi mbili za mabao.


Pia katika kabati lake kuna mpira mmoja ambao aliupata msimu huu baada ya kufunga hat trick mbele ya Coastal Union. 


Ameweza kuvunja fupa ambalo lilikuwa linawatesa wazawa kwa misimu mitatu mfululizo bila wao kusepa na tuzo ya kiatu cha ufungaji bora.


Ilikuwa ni msimu wa 2017/18 kiatu kilisepa na Emmanuel Okwi alikuwa Simba na alitupia mabao 20 kibindoni huyu ni raia wa Uganda.

Msimu wa 2019/20 alikuwa ni Meddie Kagere alifunga mabao 23 pia msimu wa 2020/21 Mnyarwanda huyu alisepa na kiatu baada ya kufunga mabao 22.

Anaitwa John Bocco leo anatimiza miaka kadhaa kwa msimu wa 2020/21 ni mfungaji bora mzawa na timu yake pia imetwaa taji la Ligi Kuu Bara.


Maisha mema John Bocco unidirectional kuwa na busara na afya tele nahodha wa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic