August 15, 2021


 MZEE wa kuchetua Bernard Morrison amesema kuwa maisha ndani ya Simba ni raha huku akifurahi uwepo wa Jonas Mkude ambaye alikuwa nje ya kikosi kwa muda kutokana na masuala ya nidhamu.

Kwa sasa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kimeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Ni mabingwa watetezi wa ligi pia walitwaa taji la Kombe la Shirikisho kwa ushindi mbele ya watani zao wa jadi Yanga kwa ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa mwisho wa reli Kigoma, Uwanja wa Lahe Tanganyika.

Morrison amesema:"Ninafurahi kuwa ndani ya Simba pia kuwa na kijana kutoka Muhimbili, Jonas Mkude hapa ni furaha kubwa ndani ya Simba.

"Ukimzungumzia Mkude unataja moja ya viungo wakabaji bora Tanzania, hivyo nipo na mchezaji bora kwenye eneo la viungo wakabaji ni furaha tupu," amesema.

Mkude kutokana na matatizo ya nidhamu ya kujirudiarudia mara kwa mara ndani ya Simba kabla ya kuepa kueleka Morocco ilielezwa kuwa alipaswa kwenda Muhimbili kufanyiwa vipimo.

Kwa sasa yupo nchini Morocco Mkude na alitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzo kuripoti kambini, Dar kabla ya timu kuelekea Morocco.

10 COMMENTS:

  1. Hiyu mkude ajifunze kuwa maisha yamebadilika sana, huo utaratibu wake wa maisha umepitwa na wakati, azingatie kazi yake. Hadi wanamtania sasa kuwa kijana wa muhimbili!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anatakiwa ajue kuwa mpira una umri, miaka haisimami,Simba Sc. ni mlezi kwake.

      Delete
  2. Wachezaji wa kitanzania hawatokaa wajitambue hata siku moja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kauli za kujumuisha wewe. Samatta, Msuva, John n.k ni WA wapi? Tabia ya mtu mmoja haiwezi ikawa tabia ya wote.

      Delete
  3. Ndiyo maana mpira wa Bongo haukui,ilitakiwa Mkude atemwe kama walivyofanya watani wetu Young kwa kumtema Metacha,kiburi hiki ndicho kinampa kiburi cha kurudia mara kwa mara utovu was nidhamu,hata ukiwa mfanyakazi bora kiasi gani displine ndiyo kila kitu katika maisha,sitashangaa akirudia upuuzi wake, maana viongozi wenyewe ndiyo wanamfuga,nidhamu keanza,Mambo mengine yanafuata

    ReplyDelete
  4. Utovu wa nidham k2 gani bana,mbna hawausemi kwa mashabik tujue sisi tuna angalia ndani ya uwanja ananidham Sana Mambo ya nje ya uwanja ni yakawaida fatilieni kwa wenzetu msiongee2

    ReplyDelete
  5. ha ha ha ha,mbwa mzee hafundishwi kuwinda?

    ReplyDelete
  6. Nidhamu ndo kila kitu.hata samata nawengineo wasingefika hapo walipo wangekosa nidham.

    ReplyDelete
  7. Mkude hata mm nampenda Sana na Ni shabiki wake,lkni ktk mpira kitu nidhamu ndio kila kitu hata uwe na kipaji kiasi gani,oneni balotel mpk sasa hatujui anacheza ligi gani ,,Ila kwa hili naona amejifunza kitu

    ReplyDelete
  8. Mkude mtu ila tadeo ni mtu na nusu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic