KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amebainisha kwamba bado timu yake haijawa na muunganiko bora licha ya kwamba ilikuwa imeweka kambi nchini Morocco.
Jana, Agosti 24 kikosi cha Yanga kilirejea Dar baada ya kuvunja kambi yao iliyokuwa nchini Morocco kwa kile walichoeleza kuwa ni maslahi mapana ya Yanga.
Maandalizi yao kuelekea msimu wa 2021/22 sasa yatakuwa ni Kigamboni katika kijiji cha Avic Town.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Nabi amesema;-“Muunganiko wa timu bado, tunahitaji muda kama mwezi au miezi mitatu kwa sababu timu haijengwi kwa muda mfupi.
"Wachezaji wote tuliowasajili ni wazuri kwa sababu tulikuwa tunawafuatilia, tukipata muda zaidi tutakuwa bora zaidi,” amesema Nabi.
Hiyo ndio kazi ya kocha
ReplyDeleteUmeanza visingizio, miezi yote hiyo c tutakuta Simba ashatangaza ubingwa
ReplyDeleteKila msimu kinacho tufelisha ni muunganiko, baadae utasikia kocha hafai wkt huo Mnyama anachanja mbuga mwisho wa siku utasikia wanabebwa
ReplyDeleteHawa hawatachukua muda mrefu kwani hawakuleta makanjanja hata mmoja
ReplyDeleteShida kubwa ilikuwa ufungaji.
ReplyDeleteMakambo na Mayele wanaweza kuanza huko.
Wengine wakacheza wale wale.
Cha haraka sana ni kupata first 11.
Ukimbwela mbwela itakula kwako Nabi.
Wakati wananunuliwa wachezaji wengi kutoka kama club moja ni kwa sababu ya kurahisisha muunganiko.
Visingizio havitakubalika.
Labda iwe mbinu ya kiukocha lakini kama kweli unahitaji miezi hadi 3,hutoboi