August 24, 2021


 TIMU ya soka ya Geita Gold ya mkoani Geita iliyopanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao, imemtambulisha aliyekuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Ettiene Ndayiragije kuwa kocha wao mkuu.

Ndayiragije baada ya kutambulishwa ndani ya kikosi hicho ameomba  kupewa ushirikiano wa timu hiyo ambapo atasaidiana na kocha Fred Felix Minziro kuelekea msimu ujao wa ligi.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Aman Nichoraus ameliambia Championi kuwa:- “Kocha Ettiene Ndayiragije amesaini mkataba wa kuinoa klabu yetu kwa muda wa miaka miwili ambapo atasaidiana na kocha aliyetupandisha daraja, Fred Felix Minziro ambapo tunaamini wataliongoza jahazi la Geita Gold kufanya vizuri kwenye ligi kuu.

“Sababu kuu za kumleta Ndayiragije ni uwezo wake aliouonyesha wakati akifundisha klabu za Tanzania kwani wote ni mashahidi kwamba wakati Ndayiragije alipokuwa kocha wa Mbao wote mliona ilivyokua ikifanya vizuri, alipoenda KMC timu ile ilibadilika na hata alipopewa kazi Azam FC bado kazi yake ilionekana kuwa kubwa mpaka kuitwa timu ya taifa hivyo sisi kaka Geita tunaamini atatusaidia," .

 

Kwa upande wake Kocha Ettiene Ndayiragije alisema: “Nawashukuru sana viongozi wa Geita kwa kuniamini na kunipa kazi sina cha kuwalipa ila nawaomba ushirikiano ili tuweze kuifanya Geita Gold kuwa timu bora," .

3 COMMENTS:

  1. Minziro kazi yake ni kusukuma gari toka kwenye matope likifika kwenye lami anapewa dereva mwingine halafu yeye anaambiwa akae seat ya nyuma kusubiri lipate pancha afungue tairi

    ReplyDelete
  2. Hongera Kocha Minziro kwa utulivu, utendaji kazi bora,uaminifu na mwenye upendo, nachukua fursa hii kusema njia ya mafanikio zaidi kwako ni kuendelea kuwa mtulivu hapo Geita Fc, kwani hakuna asiyefahamu ubora wako. Mimi naamini kwa kushirikiana na Kocha Mkuu nawe utajiendeleza zaidi na kupata mafanikio. Hongera Ndaragije kwa kurudi kufanya kazi Tanzania.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic