August 13, 2021


KIKOSI cha Yanga kinatarajiwa kuibukia nchini Morocco kwa ajili ya kuweka kambi ya muda wa siku 11 ikiwa ni maandalizi ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho pamoja na ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni nyota 28 ambao wanatarajiwa kuwa kwenye msafara wa kikosi hicho huku nyota wake Juma Makapu ambaye ni beki pamoja na mshambuliaji, Wazir Junior wakiwekwa kando kwenye mpango wa msafara huo.

Ni Diarra Djigui raia wa Mali, Erick Johora na Ramadhan Kabwili hawa ni wazawa kwa upande wa walinda milango baada ya kuachana na Metacha Mnata na Faroukh Shikalo.


Wengine ni Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu,'Ninja', Dickson Job, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Adeyum Saleh, Paul Godfrey, David Bryson ingizo jipya kutoka KMC, Djuma Shaban na Yannick Bangala kutoka DR Congo.

Mzawa Deus Kaseke, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Mapinduzi Balama, hawa nao wanatajwa kuwa kwenye msafara, Mukoko Tonombe, kutoka Congo na Khalid Aucho raia wa Uganda naye pia.

Farid Mussa, Ditram Nchimbi, Yacouba Songne, Said Ntibazonkiza, raia Burundi, Yusuf Athuman ingizo jipya kutoka Biashara United, Dickson Ambundo ingizo jipya kutoka Dodoma Jiji, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Jesus Moloko wote kutoka DR Congo.


Wanatarajiwa kuwa katika Akademi ya soka ya Mohammed VI ambapo ndani kuna majengo makubwa ya kiutawala, Hospitali, viwanja vinne vya mazoezi vya kisasa vya nyasi bandia na nyasi asilia vyenye ukubwa tofauti.


7 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic