August 14, 2021


RASMI kikosi cha Simba leo kimemtambulisha Pape Ousmane Sakho raia wa Senegal mwenye miaka 24.

Nyota huyo anakuwa ingizo jipya la nne ndani ya Simba baada ya jana Agosti 13 kumtambulisha Duncan Nyoni aliyeungana na Peter Banda pamoja na mzawa Yusuph Mhilu.

Nyota huyo anatajwa kuwa na uwezo mkubwa ndani ya uwanja pale anapopata nafasi akiwa ni kiungo mshambuliaji kinda aliyefanya vizuri kwenye ligi ya Senegal.  

Rekodi zinaonyesha kwamba alitupia mabao 8 na pasi 10 alitoa, pia ndiye mchezaji aliyeng'ara wakati timu ya Teungueth ikiitoa timu ya Raja Casablanca ya Morocco msimu ulioisha na kufuzu hatua ya makundi ya Caf Champions League.

Kwenye kambi nchini Morocco ambapo Simba wapo kwa sasa atajumuishwa na wengine ili kuendelea na maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.

7 COMMENTS:

  1. Usajili wa viwango. Hongereni simba. Vitu Kama hivi ndivyo vilivyofanya Tanzania kujulikana from nowhere in African football na Sasa tupo kwenye ramani ya soka. Jitihada zifamywe kwenye Timu ya Taifa kuendana na heshima tunayopewa Sasa kwenye ngazi ya Klabu hakuna kisichowezekana ni juzi tu watu wakisia Simba imepangwa na warabu watu wanacheka kwa dharau lakini leo warabu wanakimbia kupangwa na Simba. Kama tulikuwa gizani ndani ya handaki basi sasa Kuna mwanga unaonekana dhahiri shahiri wa kutokea. Tunachotakiwa ni kijipanga kwa timu zetu msimu huu kwenye mashindano ya kimataifa na kufanya vyema zaidi.

    ReplyDelete
  2. Usajili huu balaa maana nj watoto watupu. Umri chini ya umri wa Chama

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli yanga tumechanganyikiwa. Maana usajili wetu ni vijeba vitupu. Sijui msimu utakuwaje. Ila mimi binafsi kama mpenda maendeleo ya soka nawapa big up Simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usidanganywe na umri wa kwenye passport

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic