TABASAMU kwake ni jambo la kawaida kila wakati akiwa ameweza kuyeyusha jumla ya miaka 32 kwa neema za Mungu akiwa katika afya bora na imara zaidi ya jana.
Licha ya tabasamu lake ni katili akiwa uwanjani katika kucheka na nyavu pamoja na kuwatesa makipa wengi anaokutana nao uwanjani kwa kuwaokotesha mipira katika nyavu zao namna anavyotaka.
Anaitwa Robert Lewandowski raia wa Poland nafasi anayocheza uwanjani ni mshambuliaji wa kati ndani ya kikosi cha FC Bayern Munich ambacho kinashiriki Bundesliga.
Alijiunga na timu hiyo Julai Mosi 2014 na mkataba wake unatarajiwa kumeguka Juni 30,2023 anapenda kutumia zaidi mguu wake wa kulia.
Ana tuzo 17 za ufungaji bora kabatini mwake ambapo ile tuzo ya Bundesliga kwake imekuwa utalii kusepa nayo kwa kuwa msimu 2013/14 alitupia mabao 20, 2015/16 alitupia mabao mabao 30, 2017/18 alitupia mabao 29, 2018/19 alitupia mabao 22,2019/20 mabao 34,2020/21 alitupia mabao 41.
Tuzo 10 ni za mchezaji bora wa mwaka kuanzia 2011 mpaka 2019 alisepa na tuzo ya mchezaji bora wa Poland na 2020 na 2021 ilikuwa ni kwa nchi ya Ujerumani. Mara 9 mfululizo amenyanyua makwapwa katika German Champion akiwa na timu mbili tofauti alipokuwa na Borussia Dortmund mara mbili msimu wa 2010/11 na 2011/12 na kuanzia 2014/15 mpaka 2020/21 ametwaa taji hilo akiwa ndani ya Bayern Munich.
Ametwaa taji moja la FIFA World Cup 2021 na taji moja la UEFA Super Cup msimu wa 2020/21 yote alikuwa ndani ya Bayern Munich. Pia ametwaa taji la German Super Cup mara 5, mara moja akiwa na Dortmund msimu wa 2013/14 na mara nne mfululizo akiwa na Bayern Munich kuanzia 2016/17 mpaka 2020/21.
Rekodi zinaonyesha kuwa katika ngazi ya klabu kwenye mashindano yote tangu msimu wa 2007/08 mpaka msimu wa 2021/22 amecheza jumla ya mechi 441 na amefunga jumla ya mabao 331 na pasi 87, kadi za njano ameonyeshwa jumla 44 na nyekundu moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment