UONGOZI wa Simba umebainisha kwamba jitihada za kumbakisha nyota wao Clatous Chama ziligonga mwamba baada ya mchezaji huyo lkuomba kupata changamoto mpya.
Leo Agosti 16 baada ya tetesi kueleza kwamba Chama atakuwa ndani ya kikosi cha RB Berkane cha Morocco imetolewa taarifa rasmi kwamba Chama pamoja na mshikaji wake Luis Miqissone hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho.
Crescentius Magori Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi ya Simba amesema kuwa hawakuwa na mpango wa kumuuza Chama ila yeye mwenyewe aliomba kuondoka na pesa ambayo wamewauza wachezaji hao ni ndefu mfano wake hakuna.
"Kiasi cha pesa ambacho tumewauza Chama na Miquissone ni siri kwa sababu ni matakwa ya mkataba na klabu tulizowauzia hawakutaka tuweke wazi.
"Lakini pia klabu ambayo tumemuuza Miquissone haikutaka tutangaze kwa sababu nchini kwao bado ligi inaendelea na kuna wachezaji wa kigeni wanawategemea katika kupigania ubingwa hivyo kama tungetangaza kuwa Miquissone tumemuuza katika klabu hiyo basi ingeleta sintofahamu kwa wachezaji na kuathiri mbio zao za ubingwa.
"Dau tulilowauza limeweka historia katika nchi hii, haijawahi kutokea katika nchi hii, Miquissone ameuzwa kwa dau kubwa halijawahi kutokea, mshahara anaokwenda kulipwa hata baadhi ya wachezaji wa Ulaya hawalipwi, anaenda kulipwa mara 8 ya mshahara tuliokuwa tunamlipa.
"Chama tulikuwa tumempa mkataba wa miaka miwili ambao alikuwa analipwa mshahara mkubwa kuliko mchezaji yeyote nchi hii, mkataba huo ndio kwanza umeanza, hatukuwa na mpango wa kumuuza ilitokea tu. Mchezaji mwenyewe ndiye alipush, (lazimisha) kuondoka kutokana na mshahara.
" Chama alisema mimi hapa Simba nimefanya kila kitu, nimeifikisha Simba robo fainali Champions League mara mbili, nimekuwa MVP, umri wangu ni miaka 30, naomba nikapate malisho yaliyo bora.
"Hapo ndipo sisi washauri tukaamua kushauri mchezaji aachwe aende kwa maslahi ya mchezaji na klabu," .
Safi uongozi wa Simba. Sio sisi Yanga mchezaji akitaka kuondoka inakuwa nongwa ati utovu wa nidhamu. Ahhh hatuna weledi
ReplyDeletewe yanga gani hujui kama kisinda kauzwa unatomboka tu
DeleteMimi nawapenda Simba kwakuwa wasema kweli. Kwa kutamka kuwa hawataka kumtoa na walijaribu sana kumzuwia ni wazi walimpenda na kumtukuza na kumheshimu na hsta kuweka wazi kuwa huko anapokwenda mshahara wake ni mardufu kuliko aliokuwa anaupata Simba. Tazama namna gani Simba inavowakadiri wachezaji wake.
ReplyDeleteSafi ila chama akifail huko hasirudi maana kaondoka najua kwa kinyongo Ila Luis unakaribishwa Simba next time Kama ukipenda tofauti na hapo nakuona baada ya miaka 3 unacheza ulaya
ReplyDeleteDua la kuku......utakufa kwa kujaza vinyongo kifuani
DeleteKumtukuza? Dhuu..miungu!
ReplyDeleteEti rocord. Sasa si utangaze tujue kama ni kweli dau nono au kutaka tu sifa na kukwepa lawama
ReplyDeleteHapo Mwamedii anasemaje?
ReplyDeleteMaana pesa yote inayotumika inatoka mfukoni kwake? bado Simba inaendeshwa kwa hasara?
Chama aliomba kuondoka baada ya kudhalilishwa na tajiri kisa tu kumjibu shabiki wa Simba kwamba Haji Manara alikuwa ni mtu muhimu katika timu,hakutaka kudhalilishwa utu wake kwa sababu ya pesa.
ReplyDeleteDharau ziwe na mipaka na wenye pesa wawe na adabu.
Huu ndio ukweli
DeleteAwe ameomba ama vinginevyo kuondoka yote ni heri alimradi biashara nzuri imefanyika. Na inshallah miongoni mwa majembe mapya yaliyosajiliwa kwa msimu mpya watakuwepo walio bora zaidi ya Chama na Miqisson
ReplyDelete