BAADA ya kuwepo kwa uvumi kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutofanyika kwa tamasha la siku ya Simba ‘Simba Day’ Uongozi wa Klabu hiyo umeibuka na kuweka wazi kuwa tamasha hilo lipo.
Leo kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba umebainisha kuwa tarehe ya Simba Day itakuwa ni Septemba 19.
Kwa kawaida tamasha hilo hufanyika Agosti 8, kila mwaka ambapo kwa mwaka huu uongozi wa Simba ulilazimika kulisogeza mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ratiba ngumu ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Pre season’.
Sehemu kubwa ya kikosi cha Simba kwa sasa kipo nchini Morocco kwa ajili ya kambi ya kabla ya msimu ambayo inatarajiwa kuendelea mpaka mwishoni mwa msimu, huku nyota wengine 12 wakiwa wameitwa kwenye vikosi vya timu zao za taifa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, kuhusu tamasha hilo Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu alisema: “Kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wakijaribu kusambaza uvumi kuwa eti tamasha letu la ‘Simba Day’ lisingekuwepo mwaka huu kwa sababu mbalimbali ambazo wamezieleza, lakini nikuhakikishie kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.
“Kwa sasa menejimenti inapanga utaratibu mzima wa kufanyika kwa tukio hilo, na tutatoa taarifa rasmi juu ya utaratibu mzima wa kufanyika kwa tamasha hilo," .
0 COMMENTS:
Post a Comment