KIKOSI cha Simba kikiwa nchini Morocco ambapo kimeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 leo kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki ili kuweza kujiweka sawa zaidi.
Leo wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Olympique Club de Khouribga ambao utapigwa leo nchini Morocco.
Huu unakuwa ni mchezo wa pili wa kirafiki kwa Simba baada ya ule wa kwanza kucheza dhidi ya FAR Rabat ambayo inafundishwa na Sven Vandenbroeck ambaye aliwahi kuinoa pia Simba.
Katika mchezo wa kwanza wa kirafiki ngoma ilikamilika kwa miamba hiyo yote miwili kufungana mabao 2-2.
Maandalizi ya mpira sio ujanja ujanja wa kujificha kwenye shombwe la Manara.
ReplyDeletemsudan unateseka
DeleteKwani manara ndiye alileta mafanikio ya ya Simba uwanjani? Acheni mawazo potofu,... na ushabiki WA ajabu....na ushabiki wa kizandiki.
DeleteKufikiri kuwa mafanikio ya Simba yamepatikana kwa makelele ya Manara ni upuuzi wa akili. Simba imebadilika nakuwa Simba hii tunayoiona baada ya Mohammed Dewji kuamua kuekeza ndani ya Simba.Inashangaza kuona Manara akijipiga kifua kuwa yeye ndie alieipatia simba mafanikio, lazima atakuwa na matatizo ya akili.
ReplyDeleteunaumia ukiwa wapi??
ReplyDeleteSinba ni mnyama asietishika kwa lolote na kwa yeyote na juu ya kuwa mastaa wao karibu wote wamejiunga ba timu zao taifa, leo wanajtosa tena kwa hao waliobaki kupanbana ba timu zisizotabirika
ReplyDeleteTUMPONGEZE KOCHA NA BENCHI LOTE LA UFUNDI KWA KUIJENGA TIMU BILA YA WATU FULANI TUNAOWATEGEMEA. UTAKUWA WAKATI MZURI KWA KINA PAPE, BANDA, DUNCAN, JIMMYSON, DENIS KIBU, PATRICK MWENDA, MHILU YUSUF, BAKA INONGA, SADIO KANOUTE, WAKINA NDEMLA, AJIB, MKUDE, MUGALU, MADENGE NA WENGINEO.
DeletePoint🧏
Delete