MSHAMBULIAJI wa DC Motema Pembe ya nchini DR Congo, Kadima
Kabangu amefunguka kuwa tayari ameshamalizana na Simba na wiki hii kila kitu
kitakuwa sawa tayari kwa kutangazwa kuwa mchezaji rasmi wa Simba.
Kadima Kabangu kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba, ambao kwa sasa wametimkia
Morroco ambapo wameenda kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa
mashindano yote.
Akizungumzia dili hilo, Kabangu amesema kuwa kwa
sasa meneja wake yupo katika mazungumzo ya mwisho kumalizana na Simba hapa Tanzania, huku mwenyewe akiweka wazi kuwa anatarajia kutua nchini
wiki hii kwa ajili ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Simba.
“Meneja wangu yupo
Tanzania kwa sasa, amesema kuwa wiki hii kila kitu kitakuwa sawa, kuhusu mimi
kuja Tanzania nimeambiwa wiki hii nitasafriki kuja huko hivyo nasubiri taarifa
hiyo lakini ni uhakika.
“Tayari nimehakikishiwa na kocha wa Simba Didier Gomes kuwa
nipo kwenye mipango yake ya kuitumikia Simba, kwa ajili ya msimu ujao, hivyo
naamini hilo ndio linaenda kutokea,”amesema mshambuliaji huyo.
Karibu
ReplyDeleteMzee babaa karibu mximbazi kwa wababe wa soka tanzania
ReplyDeleteKumbe Wazaire kwenu Wazee baba,kwa Yanga wacheza Ndomboro lkn swali ni idadi inaruhusu
ReplyDeleteNimecheka, eti kwenu wazee baba kwa yanga wacheza ndombolo... Simba nguvu moja
DeleteIdadi ya sasa hivi wachezaji wa kigeni ni 12
ReplyDelete