USAJILI mzito ambao unaendelea kufanywa na Uongozi wa klabu ya Yanga umezidi kuwapa jeuri, ambapo sasa wameweka wazi kuwa wanataka kuweka rekodi ya kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Yanga mpaka sasa wamekamilisha na kuwatangaza wachezaji watano ambao ni Wakongomani, Heritier Makambo na Fiston Mayele, mshambuliaji mzawa Yusuph Athuman, kiungo Mganda, Khalid Aucho na mlinda mlango wa Mali, Djigui Diara huku ikiwa katika harakati za kuyatangaza majembe mapya Shaban Djuma, Yannick Bangala Litombo.
Yanga msimu ujao itakuwa miongoni mwa timu nne zitakazoiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kimataifa ambapo watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumzia mipango yao kuelekea michuano ya Kimataifa, Mkurugenzi wa mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro amesema: “Kikosi chetu kinaendelea kufanya usajili mkubwa kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, tayari tumewatambulisha rasmi baadhi ya wachezaji, na kuna majembe zaidi yanakuja.
“Malengo yetu ni kufanya vizuri msimu ujao kwenye michuano mbalimbali
tutakayoshiriki, lakini malengo yetu makubwa zaidi ni michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika ambapo tunataka kuandika rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na
timu za Tanzania.”
Haya bhana
ReplyDeleteTunaipenda vilabu zetu zikifika mbali sio yanga sio simba sc mana sote zinaiwakilisha Tanzania,, yoyote itakayofanikiwa Tanzania imefanikiwa
ReplyDeleteLigii za nyumban utopolo umechemka utaweza kimataifa kwa wachezaji akina makambo waliochemka horoya hawana jipya utopolo wachezaji wazuri watawapata wao
ReplyDeleteMsgazeti ndio yanayowazuzua matapolo halafu mwisho wa siku sufuri. Sasa ndio wanamini kabisa ya ubingwa wa nyumbani na ule wa Africa wakichochewa na magazeti nao wakiamini.
ReplyDelete