PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa kupoteza kwao mchezo wa Ligi ya Mabingwa mbele ya PSG ni moja ya vipindi ambavyo vinatokea kwenye mpira hivyo wanakwenda kula vizuri na kupumzika kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Liverpool.
City ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya PSG kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jambo ambalo limewafanya wawe nafasi ya tatu kwenye kundi A na pointi zao ni tatu vinara ni PSG wenye pointi nne wote wakiwa wamecheza mechi mbili.
Guardiola amesema kuwa walicheza kwa mbinu za kusaka ushindi ila kilichotokea ni uimara wa kipa wa PSG, Gianluigi Donnaruma ambaye alifanya kazi kubwa kwenye kuokoa hatari za wachezaji wake.
"Tulikuwa tunahitaji ushindi na tumecheza namna hiyo ila ni sehemu ya matokeo na huwa inatokea kwenye mpira lakini yule kipa wa PSG Donnaruma alifanya kazi yake kwa kuokoa hatari nyingi.
"Kwa matokeo ambayo yametokea hamna namna tunakwenda kupumzika vizuri, kutafuta chakula na kula vizuri pamoja na kupata muda wa kumpumzika kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Liverpool," amesema.
Oktoba 3, City iliyo nafasi ya pili na pointi zao 13 wakiwa pia ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England watakutana na Liverpool ambao ni vinara wakiwa na pointi 14 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, Uwanja wa Anfield.
0 COMMENTS:
Post a Comment