September 7, 2021

 


BAADA ya mchezo kati ya Brazil na Argentina kupigwa stop juzi, nahodha wa Argentina,  Lionel Messi amechukizwa na kitendo hicho akidai kuwa haikuwa sahihi kwani walikuwa hapo kwa siku tatu.

Mchezo huo ulipigwa stop baada ya Ofisa mmoja wa afya wa Brazil kuingia uwanjani wakati mchezo ukiendelea na kutaka baadhi ya wachezaji wa Argentina waondolewe uwanjani.

Wachezaji ambao walitakiwa kuondolewa Uwanjani ni Emiliano Martinez, Cristiano Romero, Gio Lo Celso ambao wanacheza Premier League sababu wamesafiri kutoka England na hawakukaa karantini kwa muda wa siku 14 kama ambavyo sheria za Brazil zinasema.

Messi amesema:"Walipaswa kutuondoa nchini mwao siku tatu baada ya kuwasili lakini kwa nini wasubiri mpaka mchezo uanze ndipo wafanye hivyo?

"Wangetuambia mapema hili tungejua ni namna gani mambo yangekuwa hivi watu wanatuangalia,".

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic