September 17, 2021

 


PSG haipewi nafasi kubwa ya kuweza kuwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuwa na utatu matata kwenye safu yao ya ushambuliaji ambao unaongozwa na Lionel Messi, Kylian Mbappe na Neymar.

Media za Ufaransa zimeamua kuupa jina la MNM utatu huo unaotajwa kuwa na mvuto zaidi duniani kutokana na ubora wa washambuliaji hao wanapokuwa uwanjani na tamaa yao ya kufunga mabao mengi kila wanapopata nafasi.

Mchambuzi wa masuala ya michezo Michael Owen ambaye alikuwa ni mchezaji zamani amesema kuwa uwepo wa utatu huo haina maana kwamba timu hiyo inaweza kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwani utatu huo unaifanya PSG inakuwa dhaifu.

Katika mchezo wa kwanza wa utatu huo kucheza pamoja kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Messi kuanza ilikuwa dhidi ya Club Bruges siku ya Jumatano hakuna hata mmoja aliyefunga na ubao wa Uwanja wa Jan Breydel ulisoma 1-1.

Ni Hans Vanaken alisawazisha dakika ya 27 bao la Ander Herrera wa PSG aliyepachika bao hilo dakika ya 15.Pia rekodi zinaonyesha kuwa PSG walipiga mashuti 9 na yaliyolenga langoni yalikuwa ni manne huku wapinzani wao Club Bruges wakipiga mashuti 16 na 7 yalilenga lango.

Owen amesema:"Hii timu ya PSG ina maofowadi bora sana kwa sasa lakini watatu hao pamoja wanaifanya inakuwa dhaifu na sijui kwa nini ni timu inayopewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya nadhani timu za England ni bora zaidi yao kwa mbali sana," .

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic