September 24, 2021


CEDRICK Kaze, anatarajiwa kutambulishwa muda wowote kwa mashabiki wa Yanga baada ya kutua kimyakimya usiku wa kuamkia jana, Septemba 23.


Kaze anatajwa kurejea ndani ya timu hiyo kuja kuwa msaidizi wa kocha wa sasa Nasrredine Mohamed Nabi ambaye kwa muda sasa amekuwa akifanya kazi peke yake.


Kaze aliondoka ndani ya timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita kufuatia mwendelezo wa matokeo yasiyoridhisha ambayo Yanga walikuwa wanavuna kwenye Ligi Kuu Bara.


Mmoja wa viongozi wa juu wa Yanga, ameliambia Championi Jumatano kuwa, zipo sababu za Kaze kurejeshwa Yanga ambazo ni elimu, uzoefu wa soka la Bongo na lugha.


“Leseni yake ya ukocha (leseni A ya CAF), ni sababu kubwa ya Kaze kurejeshwa Yanga. Viongozi wanaona hii itawasaidia Yanga kuwa chini ya makocha ambao wana leseni kubwa kutoka kwenye Shirikisho la Soka Afrika.


“Jambo lingine ni lugha, Kaze ni mzuri sana kwenye kuzungumza lugha nne kwa ufasaha ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa na Kirundi, ndani ya timu kuna wachezaji wenye kutumia hizo lugha zote nne.


“Hivyo itakuwa rahisi kwa Kaze kuweka daraja kati ya kocha mkuu na wachezaji, pia itapunguza gharama za kuwa na mkalimani wa timu.

“Lakini Kaze ni mzuri kwenye mbinu na mikakati, ni rahisi kwa kocha mkuu kubadilisha mbinu na mipango ya timu, programu za mazoezi punde tu anapopewa ushauri na msaidizi wake ambaye naye ni kocha mzuri.

“Kaze ameishi Tanzania akiifundisha Yanga kwa takriban miezi sita, anavijua vizuri viwanja vya mikoani, hivyo ni rahisi kumsaidia mwalimu juu ya uchaguzi wa wachezaji sahihi kwenye viwanja tofauti.”


Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro, aliliambia Championi Jumatano kuwa, wapo kwenye mchakato wa kutafuta kocha msaidizi kwa sasa ingawa siyo kweli wamemalizana na Kaze kwa sababu bodi haijakaa na kujadili suala hilo.

15 COMMENTS:

  1. Inamaana YANGA ilipokuwa ilipokuwa inamtimua Cedric Kaze katika nafasi ya ukocha Alikuwa hana ELIMU??
    Huyo kaze Alikuwa hajui kiingereza kifaransa Na KISWAHILI Na Kirundi ???
    Alikuwa havijui viwanja vya Tanzania Na sasa kaenda kusomea wapi ???
    YANGA kwanini msiseme Ukweli kuwa mlimtimua kaze bila sababu na sasa mnamrudisha tena BILA SABABU ????
    KULIKO KUDANGANYA

    ReplyDelete
  2. jamaa wanababaika Kwahakijui cha kukifanya

    ReplyDelete
  3. Hayo yote hamkuyafaham wakat mnamtimua? Uto ni uto tu

    ReplyDelete
  4. Kwani Nabi alikwepo wakati anatimuliwa? Na si anarudi kuajzia patakapopungua tu. Yaani makoro vichwa vyenu vina ndimu..hahaha

    ReplyDelete
  5. Ukiitwa utopolo pigana aisee

    ReplyDelete
  6. Je ukiitwa koro aka mikia aka paka mweusi aka vichupi..

    ReplyDelete
  7. Hii ni yanga jamani and the other side wanasema their team is Simba so wacha soka liendelee

    ReplyDelete
  8. Yanga ilikua zamani sio yanga ya sasa,imebaki kujiita timu ya wananchi wakat chenga tupu,mmetia aibu sana kwasababu katika kipindi ambacho mmejinasibu sana kwamba mko sawa na mtabeba makombe yote mpaka caf champion na mkianza na ndondo kapu kule Zanzibar,cha ajabu mnatolewa hatua za awali tena mnapigwa ndani nje na figisu zenu lakin bado mkawekwa hapahapa.poleni sana ila mngejifunza kuwaheshimu wakubwa.

    ReplyDelete
  9. Simba nguvu moja.... Kesho kwa mkapa tunapiga mtu tunatwaa kolo letu la kuanzia msimu tunaliweka kabatini huku tukiendelea kuwinda makolokolo mengine kama FA na Ligi kuu.... Sisi ndo wazee wa makolokolo kama mlikuwa hamuelewi sasa ndo muelewe maana yake leo nimeamua kuwafumbua macho UTOPOLO

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pia wajulishe kuwa leo tumesaini kolo lenye faida la mil.800 na kufanya mabasi yetu pamoja na jezi zetu kuwa na makolo mengi zaidi Simba nguvu moja mpaka wapoteane hao utops

      Delete
  10. Utopolo ni Utopolo tu, duniani hadi mbinguni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic