NYOTA wa soka nchini Cameroon, Samuel Eto’o ametangaza kugombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Cameroon. Eto’o ametoa tangazo hilo Jumanne kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook.
Nyota huyo amesema:-“Nimeamua kuchukua uamuzi huu kwasababu ya kuipenda Cameroon na kupenda soka letu. Ni wakati wa kujenga upya mpira wetu,” alielezea Eto’o katika taarifa yake hiyo.
Eto’o anaweza kukupambana na kizuizi kwa kile kinachodaiwa kuwa ana uraia pacha wa Hispania tangu wakati akicheza Barcelona.
Miongoni mwa masharti yanayotakiwa kuwa mgombea wa urais wa shirikisho la mpira wa miguu la Cameroon, ni marufuku ya kuwa na utaifa wa kigeni.
Samuel Eto’o ni kigogo wa tatu wa zamani kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon. Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa ugombea wake utathibitishwa. Uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 11.
Well done boy
ReplyDelete