October 13, 2021


 KOCHA Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema kuwa anamtambua vema mshambuliaji wake Kibu Denis hivyo ana uhakika kwamba atakuja kuwa mchezaji muhimu kwenye timu hiyo.

Kwa sasa Simba inafanya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Akizungumza na Saleh Jembe, Gomes amesema kuwa kwa namna ambavyo amemtazama Kibu akiwa kwenye timu ya taifa na muda aliokuwa nao kwenye mazoezi ni jambo ambalo linampa matumaini kwamba atafanya vizuri.

Nyota huyo ni ingizo jipya ndani ya Simba ambapo aliibuka hapo akitokea kikosi cha Mbeya City kwa dili la miaka miwili.

Gomes amesema:"Kibu ni moja ya wachezaji wazuri na amekuwa kwenye mwendo mzuri katika kutimiza majukumu yake niliweza kumuona kwenye mechi ambazo tulicheza alikuwa vizuri.

"Hata kwenye mchezo wa timu ya taifa dhidi ya Benin nimeona kwamba ana kitu ambacho amekionyesha hivyo nina amini kwamba atakuja kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi," amesema.

 Simba itakuwa na mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy Oktoba 17 ambapo inatarajia kukwea pipa Oktoba 15 kwa ndege binafsi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic