October 9, 2021


MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Benjamin Kalume amesema kuwa mpango wa uchaguzi wa viongozi wa Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) umeanza kwa mujibu wa katiba.

Kalume amesema kuwa kwa mujibu wa kanuni ya TPLB inaeleza kuwa ukomo wa uongozi ni wa muda wa miaka minne hivyo kwa sasa wanatakiwa kufanya uchaguzi kwa kuwa muda huo umekwisha.

Nafasi ambazo zinawaniwa ni pamoja na ile ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti hapa kila nafasi ni mtu mmoja huku kukiwa na nafasi ya wajumbe wawakilishi wa vilabu vya ligi kuu nafasi tatu, wajumbe wawakilishi wa vilabu Ligi Daraja la Kwanza, wajumbe wawili na mjumbe wa Ligi Daraja la pili nafasi moja.

“Gharama za fomu kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa bodi ni laki mbili, wajumbe wa kamati ya utendaji ni laki moja. Fomu zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 11-15 Oktoba na zitapatikana TFF, na tovuti yake pia.

“Kamati ya uchaguzi imeweka kalenda ya matukio mpaka kufikia uchaguzi ambao utafanyika mkoa wa Kigoma Novemba 27. 11-15 Novemba wagombea kuchukua fomu, Oktoba 16-17 kikao cha mchujo wa awali na kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali Oktoba 18-19 itakuwa ni kipindi cha kuchapisha na kubandika orodha ya awali ya wagombea, Oktoba 20-22 kipindi cha pingamizi, 23-25 Oktoba itakuwa siku ya kusikiliza mapingamizi kama yatakuwepo.

“Oktoba 26-28 usaili kwa wagombea, 29-30 itakuwa siku ya kutangaza matokeo ya awali ya usaili, Oktoba 30-11 Novemba masuala ya maadili yatawasilishwa, 3-5 Novemba kipindi cha kupokea na kutolewa maamuzi masuala ya maadili.

“6-7 Novemba itakuwa ni kutangaza matokeo kuhusu taarifa za maadili, 8-10 kipindi cha kukata rufaa, 11-13 ni kusikiliza rufaa za maadili kwa kamati ya rufaa ya TFF, 14 itakuwa ni siku ya kutoa maamuzi ya rufaa, 15-16 ni kipindi cha kukata rufani dhidi ya kamati ya uchaguzi, 17-19 rufaa kusikilizwa kamati ya uchaguzi ya TFF na Novemba 20 wagombea kujulishwa uamuzi wa rufani.

“Novemba 21 orodha ya mwisho ya wagombea kutangazwa, Novemba 25 itakuwa ni kipindi cha kampeni na Novemba 27 uchaguzi,” amesema Kalume.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic