Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema sare dhidi ya Mbeya City haiwezi kukifanya kikosi chake kuyumba kwa
kuwa wanaamini sare ni sehemu ya mchezo.
Simba imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wake Mbeya City katika mechi iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
“Kweli tumepata sare na tulichotaka ni
kushinda, vijana walijitahidi na hakuna sababu ya kukata tamaa,” alisema
Logarusic.
“Tutaendelea kupambana hadi mwisho kwa
kuwa ligi bado ina nafasi za kuendelea kushinda kama tutajiandaa vema na kuwa
makini.
“Kwetu suala la Mbeya City limepiga na
sasa tunachoangalia ni mechi inayofuata na hakuna zaidi,” alisema Logarusic.
Rekodi ya Simba katika Ligi Kuu Bara
chini ya kocha huyo inaonyesha hivi, ameiongoza katika mechi tano, ameshinda
mbili, amepoteza moja na sare mbili.







0 COMMENTS:
Post a Comment