August 27, 2014



Andrey Coutinho amewatoa hofu Yanga kwamba ana uwezo tofauti na walivyokuwa wakimfikiria baada ya kufunga bao saaafi katika mechi ya kirafiki dhidi ya KMKM wakati Yanga ikishinda kwa mabao 2-0, usiku huu.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa, Coutinho raia wa Brazil alipiga bao hilo baada ya kupokea pasi ya Mrisho Ngassa katika dakika ya 44.
Baada ya kupokea pasi hiyo umbali wa takribani mita 27, alizuga kama anatoa pasi, akiwa ameangalia upande mwingine aliusogeza mpira mbele na kupiga shuti kali lililojaa wavuni.
Coutinho alishindwa kujizuia baada ya kufunga bao hilo na kuvua jezi yake kwa furaha huku wachezaji wenzake wakimshangilia kwa nguvu.
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili KMKM walijitutumua na kupeleka mashambulizi mengi, lakini Yanga walikuwa imara zaidi.
Yanga walipoteza nafasi kadhaa lakini huku baadhi ya mashabiki wakiwa wameanza kutoka nje wakiamini Yanga imeshinda kwa bao hilo moja, Hussein Javu alifunga bao la pili kwa shuti kali pia, hiyo ikiwa ni dakika ya 90.


Jerry Tegete ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Javu alipoteza nafasi kadhaa za kufunga. Naye Hamisi Kiiza na Amos Abel, nafasi zao zilichukuliwa na Said Bahanuzi na Edward Charles.
Kikosi:

Huo unakuwa mchezo wa tatu wa kirafiki kwa Yanga kukipiga Zanzibar na imeshinda yote.
Ilianza na Chipukizi na kushinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Jaja kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Ikapaa hadi Unguja na kuichapa Shangani kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Hivyo imeshinda mchezo mmoja kisiwani Pemba na miwili kisiwani Unguja.

Kikosi:
Deo Munishi ‘Dida’/Juma Kaseja (Dk46), Salum Telela/Said Juma (Dk46), Oscar Joshua/Amos Abel (Dk46)/Edward Charles (Dk70), Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Rajab Zahir (Dk46), Mbuyu Twite/Omega Seme (Dk46), Mrisho Ngassa/Simon Msuva (Dk46), Hassan Dilunga/Nizar Khalfan (Dk46), Geilson Santana ‘Jaja’/Jerry Tegete (Dk46/Said Bahanuzi (Dk70), Haruna Niyonzima/Hamisi Thabiti (Dk46) na Andrey Coutinho/Hamisi Kiiza/Hussein Javu. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic