August 27, 2014



Kiungo nyota wa zamani wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ ameibuka na kuvunja ukimya kuhusiana na suala la timu gani ataichezea msimu ujao.
Dirisha la usajili wa Ligi Kuu Bara linafungwa leo saa 5:59.

Chuji amefanya mahojiano na SALEHJEMBE na kusema hana mpango wa kusajili Mwadui FC ya Shinyanga kama ambavyo imekuwa ikielezwa.
MWadui FC inafundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
“Anayesema nimesajili Mwadui ni nani, mimi nasikia habari hizo watu wanasema.
“Nilikuwa nafanya mazoezi na veterani, hata kama nilifanya na Mwadui lakini sijazungumza na kiongozi yoyote wa Mwadui wala sina mpango wa kusajili.
“Kwa kifupi sijasajili timu yoyote ya Tanzania, hivyo naomba watu wasubiri,” alisema Chuji akijiamini.
Hata hivyo, blog hii ilishaandika taarifa za Chuji kutaka kwenda kukipiga Uarabuni ambako amepata timu.
“Bado kuna mambo ninafanya, baada ya kukamilika nitaeleza, ndiyo maana ninashangazwa na taarifa hizo za kuichezea Mwadui,” alisema kiungo huyo ambaye msimu uliopita, Yanga iliamua kumuacha na kusababisha baadhi ya wajumbe wa kamati ya usajili na ile ya mashindano ya Yanga, kugawanyika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic