August 27, 2014


 Arsenal imefanikiwa kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi baada ya kuishinda Besiktas ya Uturuki kwa bao 1-0.

Alexis Sanchez aliyejiunga na timu hiyo akitokea Barcelona, ndiye ameibuka shujaa baada ya kufunga bao hilo pekee baada ya kupata pasi ya Jack Wilshere.


Arsenal iliyokuwa nyumbani iliyokuwa nyumbani ililazimika kufanya kazi ya ziada kuwafunga Waturuki hao ambao ilitoka nao sare kwao.
Licha ya kuwa pungufu baada ya beki wake Mathieu Debuchy kulambwa kadi nyekundu, Arsenal ilipambana vilivyo.
Huu ni msimu wa saba mfululizo Arsenal inafanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, michuano ambayo hugombewa na kila timu ya Ulaya.











0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic