September 1, 2014



Manchester United imeshinda vita ya kumsajili mshambuliaji wa AS Monao, Radamel Falcao.
Falcao raia wa Colombia ataichezea Man United kwa mkopo kwa msimu mmoja tu na zimetumika pauni milioni 12 kumnasa.

Mshambuliaji huyo anatua Man United kwenye siku ya mwisho wa dirisha la usajili ikiwa ni siku moja pia baada ya taarifa za yeye kutaka kujiunga na Real Madrid kuzagaa lakini baadaye akazikanusha.
Falcao mwenye umri wa miaka 28 atakuwa analipwa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki.

Wengine ambao imewasajili Man United kwa ajili ya kujiimarisha ni Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo ambao wanaungana na kocha mpya Louis van Gaal.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic