Manchester United imeshinda vita ya kumsajili mshambuliaji wa AS Monao, Radamel
Falcao.
Falcao raia wa Colombia ataichezea Man United kwa mkopo kwa msimu mmoja
tu na zimetumika pauni milioni 12 kumnasa.
Mshambuliaji huyo anatua Man United kwenye siku ya mwisho wa dirisha la
usajili ikiwa ni siku moja pia baada ya taarifa za yeye kutaka kujiunga na Real
Madrid kuzagaa lakini baadaye akazikanusha.
Falcao mwenye umri wa miaka 28 atakuwa analipwa mshahara wa pauni 200,000
kwa wiki.
Wengine ambao imewasajili Man United kwa ajili ya kujiimarisha ni Angel
di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo ambao wanaungana
na kocha mpya Louis van Gaal.
0 COMMENTS:
Post a Comment