Baada ya kuongoza kwa mabao 3-1, Man United imejikutwa ikichapwa
mabao 5-3 na Leicester City.
Katika mechi hiyo ya ugenini ya Ligi Kuu England, Man United
ilianza kupata mabao yake kupitia kwa van Persie, Di Maria na Ander Herera.
Lakini taratibu Leicester wakaanza kurudisha kama utani.
Alianza Leonardo Ulloa, akafuatia David Nugent, mkongwe Cambiaso
halafu Jamier Vardy kabla ya Ulloa kumaliza kazi kwa penalti tena.
Kocha Louis van Gaal na msaidizi wake, Ryan Giggs walionekana
hawaamini kilichokuwa kinatokea.
Beki Blackett wa Man United ambaye alionekana kuchemsha zaidi,
alilambwa kadi nyekundu.
0 COMMENTS:
Post a Comment