June 20, 2017Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza shabiki mkubwa wa Yanga, Ally Yanga amefariki dunia.


Taarifa zinaeleza, Ally Yanga amefariki dunia katika ajali ya gari huko Mpwapwa mkoani Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amethibitisha kwamba ajali hiyo imetokea leo mchana na Ally amepoteza maisha.

Ally Yanga anakumbukwa kutokana na mbwembwe zake kila Yanga ilipokuwa inacheza.

Alipenda kujipaka masizi meusi huku akiweka kitambi cha bandia.

3 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV