October 31, 2014


Siku chache baada ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka saba, Damas Ndumbaro ambaye kitaaluma ni wakili, ametamka kwa kujiamini: “Nilikaa kimya makusudi, sasa wakati muafaka umefika kuzungumzia hilo.”


Dk Ndumbaro ambaye alifungiwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kudaiwa kukiuka kanuni kadhaa za soka, anajiandaa kuweka wazi msimamo wake kuhusu adhabu aliyopewa, saa 5 asubuhi leo Ijumaa.

Dk Ndumbaro amesema kuwa amejipanga kupambana kwa hoja na kamati hiyo iliyo chini ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.

“Nilibanwa na majukumu, pia sikupenda malumbano, ndiyo maana nikawa kimya, taarifa zao nilizipata muda mrefu sana.

“Kesho njoo kwenye mkutano wangu nitazungumza kila kitu, maana unajua walitoa maamuzi nikiwa sipo, sasa muda umefika wa kufunguka,” alisema Ndumbaro.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic