October 17, 2014

TULLY (KULIA), AKIZUNGUMZA NA KOCHA MKUU WA ORLANDO PIRATES, VLADIMIR VERMOZOVIC RAIA WA SERBIA.

Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully amesema wao wana kikosi bora kuliko Yanga kutokana na sababu tatu alizozitaja.


Moja:
Tully amesema wanakutana na kikosi cha Yanga chenye beki mbovu ambayo imeruhusu bao katika kila mechi ikianza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mbili:
Yanga imepoteza mechi moja, Simba haijapoteza hata moja, ingawa imetoa sare mechi tatu.

Tatu:
Yanga wana fowadi iliyofunga mabao manne katika mechi tatu, haikufunga katika mechi moja, hivyo si ya kuilinganisha na ile ya Simba iliyofunga bao kila mechi.

Tully ametamba kwamba Simba imekuwa ikiinyanyasa Yanga inavyotaka kwa kuwa ina kikosi bora.

"Tunaiheshimu Yanga kama mtani wa jadi, lakini sisi tunajiamini kuwa kikosi chetu ni bora zaidi ya Yanga, nazungumzia kwa maana ya ufundi na si ushabiki.
"Hilo linajulikana na liko wazi, mashabiki wa Simba waje uwanjani kesho, kikubwa waiiunge timu mkono," alijigamba Tully.

Mjumbe huyo wa kamati ya utendaji alikuwa mmoja wa viongozi walioambatana na timu nchini Afrika Kusini ilikoweka kambi na kucheza mechi tatu za kirafiki ikipoteza mbili na kutoka sare moja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic