Beki wa Simba, Nassor Masoud ‘Chollo’ na kiungo mshambulizi, Paul Kiongera wameanza kufanya mazoezi mepesi ya gym huku wakiendelea na
matibabu ili kuhakikisha wanarejea katika afya zao na kurudi tena uwanjani kwa
mara nyingine.
Wachezaji hao walipata majeraha kwa nyakati
tofauti katika mechi za awali za ligi kuu, Chollo alivunjika mkono katika
mchezo dhidi ya Polisi Moro na Kiongera aliumia goti kwenye mechi dhidi ya
Coastal Union.
Msemaji wa Simba, Humphrey Nyasio, amesema kuwa maendeleo ya wachezaji wao kidogo
yameanza kutoa matumaini ingawa hawatacheza mchezo wa leo.
“Chollo na Kiongera wanaendelea na mazoezi
mepesi ya gym lakini bado hawajamaliza matibabu yao kwa sababu kama Chollo bado
hajatolewa plasta ngumu (POP), zaidi anafanya mazoezi ya kukimbia pekee na
Kiongera pia anafanya lakini anahudhuria kliniki pale Muhimbili kama kawaida.
“Lakini lengo letu ni kutaka kuhakikisha kuwa
wanapona kabisa na kurejea tena uwanjani kwa sababu bado wanahitaji uangalizi kwa
kiasi kikubwa,” alisema Nyasio.
0 COMMENTS:
Post a Comment