November 21, 2014


Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas hakuitwa kwenye timu ya taifa ya Hispania kutokana na kuwa majeruhi.

Hivyo akaamua kumchukua mpenzi wake Daniella Semaan na shemeji yake mpenzi na mzazi mwenzake wa Lionel Messi, Antonella Roccuzzo wakaenda kula bata.

Watatu hao walionekana wakitoka kwenye mgahawa mmoja wa jijini London, wakiwa na furaha kubwa.
Antonella ni mpenzi wa siku nyingi wa Messi na wamezaa mtoto mmoja.
Mwanamama huyo ni rafiki mkubwa wa Daniella ambaye ni mpenzi wa Fabregas.
Picha walizopigwa, walionyesha ni wenye furaha kubwa na ilielezwa Antonella alikuwa London kumshuhudia Messi akiichezea Argentina dhidi ya Croatia.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic