Pamoja na mambo kumuendea
vibaya akiwa na Man United, mambo yamezidi kumkaba kiungo Anderson.
Anderson ameamua kurejea
Brazil na kujiunga na timu ya Internacional lakini juzi alijikuta akitolewa
katika dakika ya 36 kutokana na kushindwa kupumua.
Kiungo huyo alitolewa
kutokana na kuwa na matatizo ya kupumua kutokana na hali ya hewa ya eneo hilo
wakati wakiivaa timu ya nchini Bolivia.
Bolivia imekuwa ikiwasumbua
wanasoka wengi katika suala la pumzi kwa kuwa iko juu sana kutoka usawa wa
bahari.
Baada ya kutolewa nje
katika mechi hiyo ya Copa Libertadores, Anderson aliwekewa mashine ya kumsaidia
kupumua.













0 COMMENTS:
Post a Comment