February 28, 2015

BANDA (KUSHOTO) ATAKOSEKANA, JOSEPH OWINO (KULIA) ATACHUKUA NAFASI YA JUUKO MURISHID.

Simba inashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, leo kucheza na Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara lakini itawakosa nyota wake wanne tegemeo.


Simba ambayo inasaka ushindi baada ya mchezo uliopita kupoteza dhidi ya Stand United, ipo kwenye mazingira magumu ya kuchukua ubingwa kwani mpaka sasa katika michezo yake 15 iliyoshuka uwanjani, imefanikiwa kushinda nne, sare nane na kupoteza tatu.

Wachezaji ambao wanatarajiwa kukosekana kwenye mchezo huo ni beki Mganda, Juuko Murshid, washambuliaji Ibrahim Ajibu na Simon Sserunkuma na kiungo Abdi Banda, wote wakikabiliwa na sababu tofauti.

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amesema kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo kubwa kwao kwani mchezo huo ni muhimu lakini anashukuru Mungu kwa kuwa kuna wachezaji tayari wameandaliwa kwa ajili ya kuziba nafasi zao na watahakikisha wanatimiza lengo lao la kubakiza pointi tatu nyumbani ili waweze kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi ambapo sasa wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 20.

“Juuko ana maumivu ya nyama za paja, Ajibu na Banda wana kadi tatu za njano wakati Simon amerejea kwao kwenye msiba wa mama yake huko Kampala, Uganda.


“Nasikitika kwa kuwa nitawakosa wachezaji hao lakini sina jinsi, nitakachokifanya ni kuyaziba mapengo yao na ninaamini nitafanikiwa kuibuka na ushindi kesho (leo),” alisema Kopunovic.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic