BANDA (KUSHOTO) ATAKOSEKANA, JOSEPH OWINO (KULIA) ATACHUKUA NAFASI YA JUUKO MURISHID. |
Simba inashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, leo kucheza na Prisons katika
mchezo wa Ligi Kuu Bara lakini itawakosa nyota wake wanne tegemeo.
Simba
ambayo inasaka ushindi baada ya mchezo uliopita kupoteza dhidi ya Stand United,
ipo kwenye mazingira magumu ya kuchukua ubingwa kwani mpaka sasa katika michezo
yake 15 iliyoshuka uwanjani, imefanikiwa kushinda nne, sare nane na kupoteza
tatu.
Wachezaji
ambao wanatarajiwa kukosekana kwenye mchezo huo ni beki Mganda, Juuko Murshid, washambuliaji
Ibrahim Ajibu na Simon Sserunkuma na kiungo Abdi Banda, wote wakikabiliwa na
sababu tofauti.
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic
amesema kukosekana kwa wachezaji hao ni pigo kubwa kwao kwani mchezo huo ni
muhimu lakini anashukuru Mungu kwa kuwa kuna wachezaji tayari wameandaliwa kwa
ajili ya kuziba nafasi zao na watahakikisha wanatimiza lengo lao la kubakiza
pointi tatu nyumbani ili waweze kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa
ligi ambapo sasa wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 20.
“Juuko
ana maumivu ya nyama za paja, Ajibu na Banda wana kadi tatu za njano wakati
Simon amerejea kwao kwenye msiba wa mama yake huko Kampala, Uganda.
“Nasikitika
kwa kuwa nitawakosa wachezaji hao lakini sina jinsi, nitakachokifanya ni kuyaziba
mapengo yao na ninaamini nitafanikiwa kuibuka na ushindi kesho (leo),” alisema
Kopunovic.
0 COMMENTS:
Post a Comment