Wanachama
na viongozi wa Klabu ya Simba, wanatarajia kukutana kesho Jumapili saa nne
asubuhi katika mkutano mkuu utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay
jijini Dar ili kuweka mambo sawa.
Simba
ipo nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 20 ikiwa imefungwa
mabao 12 na kufunga 15 ikiwa imetoa sare michezo nane na kupoteza michezo mitatu na kushinda minne katika
ligi.
Rais
wa Simba, Evans Aveva, amefunguka kuwa, ajenda watakayokwenda kuijadili katika
mkutano huo ni kuhusu mwenendo wa timu hiyo katika ligi kwa lengo la kuikwamua
timu ili iwe na kiwango kizuri katika mechi zinazofuata.
Alisema
mkutano huo utakuwa wa kawaida na watahakikisha wanatoa nafasi kwa kila mtu
kutoa ya moyoni kwa lengo la kujenga.
“Mkutano wetu upo palepale na unatarajia
kufanyika saa nne asubuhi Jumapili katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay ambapo
ajenda itakuwa moja tu ya kujadili juu ya mwenendo wa timu yetu kwenye ligi.
“Tunahitaji
kuijenga timu ili iweze kuwa vizuri, hivyo ni wajibu wa wanachama wote kujitokeza
na kujadili suala hilo kwa kina na kuleta umoja,” alisema Aveva.
0 COMMENTS:
Post a Comment