March 28, 2015


Kipa Hussein Sharrif ‘Casillas’, hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba lakini kocha wake Goran Kopunovic amempa mbinu za kucheza ‘first eleven’.


Kwa muda mrefu Casillas alikuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya ugoko aliyoyapata Afrika Kusini wakati Simba ikijiandaa na mechi dhidi ya Yanga, Oktoba, mwaka jana, hata alipopona hivi karibuni amekuwa hana nafasi kikosini.

Kuhusu kipa huyo, Kopunovic amesema: “Kwanza Casillas anatakiwa atambue mechi zilizobaki katika ligi ni chache, akitaka kucheza kikosi cha kwanza, anapaswa kujituma.

“Kujituma ndiyo mbinu pekee itakayomfanya Casillas acheze kikosi cha kwanza, kwani kinyume na hapo hataweza kupata nafasi, maana wenzake wanajitahidi.”

Simba ina makipa wanne ambao ni Ivo Mapunda ambaye ni namba moja, Manyika Peter (namba mbili), Denis Richard na mwenyewe Casillas.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic