Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amekiri ana
kibarua kigumu kuhakikisha Coastal Union inafanya vizuri katika Ligi Kuu Bara
tangu alipokabidhiwa mikoba ya James Nandwa aliyetimka.
Katika msimamo wa ligi kuu, Coastal ipo nafasi
ya tano ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 20, ikiwa imefunga mabao 14
na kufungwa 14 na mechi ijayo itacheza na Prisons Aprili 4, mwaka huu kwenye
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Julio amesema anashukuru CV yake inaendelea
kukua, lakini kwa sasa ana kibarua kigumu kuhakikisha Coastal inashika moja
kati ya nafasi tatu za juu.
“Najua nakuza CV nikiwa na Coastal, lakini
hilo litakuja baada ya kufanya kazi ngumu kwa maana ligi ni ngumu na natakiwa
kupambana ili nipate matokeo mazuri,” alisema Julio ambaye ni kocha wa zamani
wa Simba.
Julio anaifundisha Coastal kwa muda kwani ligi
ikiisha atarejea Mwadui FC ya Shinyanga ambayo hivi karibuni aliipandisha
daraja hadi ligi kuu. Zipo timu kadhaa zinazomwania Julio lakini mwenyewe
amezikatalia.
0 COMMENTS:
Post a Comment