March 29, 2015



Shuti safi la Mbwana Samatta limeiwezesha Taifa Stars kuokoka na aibu baada ya kupata sare ya mabao 1-1 dhidi ya Malawi.


Katika mechi hiyo ya kirafiki iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Malawi walipata bao lao mapema katika dakika ya 3 kupitia kwa Esau Kanyenda.

Kanyenda alifunga bao hilo baada ya kipa Mwadini Ally kushindwa kuupangua mpira vizuri. Halafu mabeki nao wakashindwa kuondosha hatari.

Stars ilishindwa kucheza vizuri hadi kipindi cha pili Mrisho Ngassa na Salum Abubakari ‘Sure Boy’ wakichukua nafasi za Harun Chanongo na Amri Kiemba.

Samatta alifunga bao hilo baada ya pasi nzuri ya Ngassa ambaye alimpiga chenga beki mmoja na kupiga krosi safi ya chinichini.


Mechi hiyo ilikuwa katika kalenda ya mechi ya kirafiki ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic