Shuti safi la Mbwana
Samatta limeiwezesha Taifa Stars kuokoka na aibu baada ya kupata sare ya mabao
1-1 dhidi ya Malawi.
Katika mechi hiyo ya
kirafiki iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Malawi
walipata bao lao mapema katika dakika ya 3 kupitia kwa Esau Kanyenda.
Kanyenda alifunga bao
hilo baada ya kipa Mwadini Ally kushindwa kuupangua mpira vizuri. Halafu mabeki
nao wakashindwa kuondosha hatari.
Stars ilishindwa
kucheza vizuri hadi kipindi cha pili Mrisho Ngassa na Salum Abubakari ‘Sure Boy’
wakichukua nafasi za Harun Chanongo na Amri Kiemba.
Samatta alifunga bao
hilo baada ya pasi nzuri ya Ngassa ambaye alimpiga chenga beki mmoja na kupiga
krosi safi ya chinichini.
Mechi hiyo ilikuwa
katika kalenda ya mechi ya kirafiki ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
0 COMMENTS:
Post a Comment