March 31, 2015

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameendelea kulifanyia kazi kwa vitendo suala la wachezaji wake kupoteza nafasi nyingi.


Kocha huyo raia wa Uholanzi, amekuwa akiwaonyesha wachezaji wake wanastahili vipi kupiga mipira.

Pluijm amesema iwapo watakuwa na uwezo wa kutumia nafasi, basi watafika mbali.
“Nafasi tunazotengeneza ni nyingi sana. Hivyo tunastahili kuzitumia kwa faida yetu.,

“Unapokosa nafasi kwa asilimia zaidi ya hamsini, maana yake hauko makini. Sasa lazima tuwe makini na kuzitumia,” alisema Pluijm.

Mara kadhaa, Mholanzi huyo alikuwa akiwaonyesha wachezaji wake namna ya upigaji sahihi na kufunga.
Pluijm ambaye amewahi kuidakia timu ya taifa ya Uholanzi, aliwataka wachezaji waongeze umakini.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic