Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Soka (TFF), inatarajiwa kukutana jumapili tarehe
24, Mei mwaka huu ikiwa ni kikao cha kawaida cha kamati hiyo.
Moja ya ajenda katika
kikao hicho itakua ni kupokea na kujadili mienendo, maandalizi na maendeleo ya
timu zaetu za Taifa za mpira wa miguu nchini.
Taarifa za ndani za TFF
zimeeleza pia kutakuwa na mjadala kuhusiaan na utendaji wa Kocha Mart Nooij wa
Taifa Stars.
Stars imeonekana kutokuwa na mwenendo mzuri
chini ya Kocha huyo Mholanzi.
Mfano mzuri ni michuano ya Cosafa ambako
tayari imecheza mechi mbili na kufungwa zote.
0 COMMENTS:
Post a Comment