March 25, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu hatma ya kipa wao namba moja Metacha Mnata kwa kuwa bado ni mali yao kwa sasa.

 Mnata kwa sasa yupo ndani ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo ilikuwa kambi nchini Kenya na leo Machi 25 ina kazi ya kumenyana na Equatorial Guinea kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON.

 

Ndani ya Yanga, msimu wa 2020/21 Mnata amekusanya jumla ya clean sheet 11 alikuwa anatajwa kuondoka ndani ya timu hiyo huku watani zao wa jadi Simba wakitajwa kuitaka saini yao.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kuwa hakuna tatizo lolote kati yao Yanga na Mnata wanachojua wao ni mchezaji halali wa timu hiyo.


“Hakuna tatizo lolote kati ya Yanga na Mnata, yeye ni mchezaji wetu na kwa sasa yupo kambini na timu ya taifa ya Tanzania hivyo mashabiki wasiwe na mashaka,” alisema.


Mnata aliibuka ndani ya Yanga akitokea Klabu ya Mbao FC ya Mwanza ambapo huko alikuwa kwa mkopo kutoka Azam FC.

9 COMMENTS:

  1. Mwache aende zake,kaihujumu yanga

    ReplyDelete
  2. muda wake kwa yabga baki miezi sita ambapo sheria inaruhusu kufanya mazugumzo kuhamia anapotaka yeye mwenyewe na ikiwa ni kweli Simba. inamtaka hakuna ataeweza kuzuwia

    ReplyDelete
  3. Viongozi huenda wanakosea Sana ndo maana Yanga haisongi aondoke tu

    ReplyDelete
  4. Mapepe huyu hafai, mchezaji Muungwana hawezi kugima Kati ya msomi, aende tu, Hana kiwango hicho bado wa kawaida sana.

    ReplyDelete
  5. Mchezaji Muungwana hawezi kugoma Kati Kati ya msimu.
    Itakuwa anamatatizo

    ReplyDelete
  6. Tuemekwisha na kutokana na hayo matamshi yetu tujuwe watatukimbia Mmoja na wakifuatia wengine kwasababu ya ndimi zetu wenyewe na hakuna mchawi isipokuwa sisi wenyewe na inawezekana haya yamepangwa na wasiotutakia mema

    ReplyDelete
  7. 👆👆 wanajitopolo wenyewe maji yashingo

    ReplyDelete
  8. Hana kiwango cha kucheza Simba ya sasa hivi. Viongozi wa Simba wakimsajili nitawashangaa sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic